Majaliwa Aagiza Uhamiaji Kuzuia Paspoti za Wafanyakazi Gas Entec Wajenga Meli

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua Ujenzi wa Meli mpya ya Mv.Mwanza Hapa Kazi tu katika Bandari ya Mwanza Kusini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mwanza kuzishikilia paspoti za wafanyakazi wa Kampuni ya Gas Entec Shipbuilding Engineering inayojenga Meli mpya ya Mv.Mwanza Hapa Kazi tu katika Bandari ya Mwanza Kusini ambayo itagharimu zaidi ya shilingi billion 97 ambapo mpaka sasa Serikali imelipa zaidi ya asilimia 80 ya fedha zote.


Mkandarasi wa mradi huu amefukuza wafanyakazi zaidi ya 100 na kubaki na wafanyakazi 20 tu

Majaliwa amesema lengo la kuchukua uamuzi unatokana na Kampuni hiyo kuondoa wafanyakazi zaidi ya 100 waliokuwa wanajenga Meli hiyo na kubakiza wafanyakazi 20 jambo lingine ni Kampuni hiyo kuuza hisa kwa Kampuni nyingine bila Serikali kujua jambo ambalo ni kinyume na mkataba wa Kampuni hiyo na Serikali ya Tanzania.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad