5/22/2022

Majizo Atoa Sababu za Kuhairisha Tamasha la Harmonize la Afro East Carnival

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Mmiliki wa Vituo vya kurushia matangazo vya EFM,E Digital na TV E (Vyombo vya habari), @majizzo ameweka wazi ni kwanini Tamasha la @afroeastcarnival la @harmonize_tz ambalo lilipangwa kufanyika 29 Mei, kuahirishwa. Majizzo ameandika

“Tumeshirikiana na @harmonize_tz kuandaa Afro East Carnival. Nampongeza sana Harmonize, yeye kama sehemu muhimu ya tukio hili amekamilisha kila alilotakiwa kufanya, na sisi wadau wengine tumefanya asilimia kubwa ya wajibu wetu.

Lakini binafsi nimetafakari tena, nimepata kiu ya kufanya jambo kubwa zaidi ya tulilokuwa tumepanga. Nimeona haja ya kuongeza vitu.

Litakuwa tamasha kubwa sana, na mimi ni tukio langu la kwanza ambalo linahusu muziki moja kwa moja kulifanya kwenye uwanja wa Uhuru. Hivyo kweli natamani makubwa zaidi : Stage kubwa zaidi, Sound na kila kitu, lakini kuwapa marafiki zetu wa Kimataifa nafasi ya kutuletea show kubwa zaidi.

Nashukuru Konde amenielewa, tumaehirisha Afro East Carnival. Tutafanya TAREHE 02/7.


Tunaomba radhi kwa kuwasubirisha ila ni kwamba nia njema zaidi🙏🏻”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger