Manara na Barbara Watinga TFF, Wahojiwa na Kamati ya Maadili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MKURUGENZI wa Klabu ya Simba Barbara Gonzalez na Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara leo wametinga katika Ofisi za TFF ambapo waliiitwa kwa aili ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya TFF.

Baada ya kutoka kuhojiwa na Kamati ya Maadili, CEO Barbara alisema kwa sasa hawezi kuongea chochote kwani wenye mamlaka ya kutoa tamko ni TFF.

Naye Haji Manara kwa upande wake alisema wamekatazwa kuongea chochote hivyo hawezi kusema chochote na amesisitiza hakuna ugomvi kati yao.

Barbara aliandikiwa barua ya kufika leo katika Ofisi za TFF akiwa na tuhuma ya kufanya mahojiano na Chombo cha Habari cha nchini Afrika Kusini cha Metro na kutamka baadhi ya maneno ambayo yanasemekana kuwa na ukakasi wa kuichafua Nchi, Klabu ya Yanga pamoja na Mpira wa Miguu wa Tanzania kwa ujumla.


Msemaji wa Yanga Haji Manara akiwa katika Ofisi za TFF
Kwa upande wake Haji Manara sababu ya wito wake haijawekwa wazi hadi sasa ingawa ni kweli kwamba wote wametinga katika Ofisi za TFF na tayari wamehojiwa na kamati ya Maadili ya TFF.

Kinachosubiriwa ni kuona je Kamati ya Maadili ya TFF itatoa uamuzi gani juu ya masuala waliyowaitia CEO Barbara pamoja na Msemaji wa Yanga Haji Manara
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad