5/18/2022

Marekani yakanusha kumuwekea vikwazo mpenzi wa Putin

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


MSEMAJI wa Ikulu ya White House anayefahamika kwa jina la Jen Psaki amesema kuwa Marekani imekanusha katika taarifa siku ya jumatatu tarehe 25 Aprili 2022 ,kwa waandishi wa habari kwamba imesitisha makusudi kumuwekea vikwazo mwanamke anayesemekana kuwa mpenzi wa Putin. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Wall Street Journal ,maafisa wa Marekani wamezuia vikwazo kwa Kabaeva kutokana na wasiwasi kwamba Putina anaweza kuliona kama shambulio binafsi.

‘’Hakuna aliye salama kutokana na vikwazo vyetu’’Psaki alisema ‘’Tayari tumemuidhinisha Raisi Putin, lakini binti yake na wasaidizi wa karibu tutaendelea kukagua zaidi,’’aliongeza.

Hata hivyo kumekuwa na wito kwa Marekani , kumuwekea vikwazo mchezaji Kabaeva mwenye umri wa miaka 38 ambaye ni mshindi wa medali ya dhahabu ya Olimpiki, kama Marekani ilivyowafanyia mabinti wawili wa Putin.

Aidha inaweza kuonekana kama ‘’pigo binafsi kwa Putini kwasababu inaweza kuongeza mvutano kati ya Urusi na Marekani ‘’ jarida hilo liliandika
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger