5/25/2022

MAUAJI...Kijana Aua Wanafunzi 19, Walimu wawili Kwa Kutumia Bunduki

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Texas, Marekani. Wanafunzi 19 na waalimu wawili wamefariki dunia kwa kupigwa risasi baada ya mtu mmoja kufanya shambulizi katika shule ya msingi kusini mwa Texas nchini Marekani.

Maofisa wa usalama wamesema kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18 alifyatua risasi katika shule hiyo kabla ya kuuawa na polisi.

Taarifa zinasema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amejihami kwa bunduki yenye uwezo wa juu.

Kabla ya kufanya shambulizi hilo katika shule hiyto, kijana huyo anadaiwa kumpiga risasi bibi yake.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa huenda alikuwa mwanafunzi wa shule ya upili katika eneo hilo.

Mkuu wa Polisi wa mji wa Uvalde ambako shule hiyo ilipo, Pete Arredondo amesema mauaji hayo yalifanyika Jumanne Mei 24, 2022 na kwamba kijana huyo alifanya shambulizi hilo peke yake.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger