5/04/2022

Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima Atoa Laki Moja Kwa Kila Aliyekatwa Mapanga na Panya Road


Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima, ametoa pole ya shilingi laki moja kwa kila mwananchi aliyekatwa mapanga katika mtaa wa Mtongani Kunduchi, Dar es Salaam usiku wa kuamkia Mei 2, 2022.

Kiasi hicho cha pesa amekitoa leo Mei 4, 2022, baada ya mbunge huyo pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, kwenda kuwatembelea na kuwajulia hali waliojeruhiwa na vijana hao.

Jumla ya wananchi 19 katika mtaa huo walijeruhiwa kwa mapanga na vijana wanaodaiwa kuwa ni Panya road usiku wa kuamkia Mei 2, 2022.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger