5/31/2022

Mchazaji Shomari Kapombe Aondolewa Taifa Stars

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Beki wa Kulia wa Simba SC Shomari Kapombe ameondolewa kwenye kikosi Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kinachojiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Afrika ‘AFCON 2023’.

Stars itacheza ugenini Juni 04 nchini Benin dhidi ya Niger, kisha itarejea nyumbani Dar es salaam kucheza dhidi ya Algeria Juni 08.

Kapombe ameondolewa kwenye kikosi hicho kutokana na kusumbuliwa na majeraha alioyapata katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold FC uliomalizika kwa sare ya 1-1 jijini Mwanza.

Maumivu hayo yalimfanya Kapombe kukosa mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Young Africans uliochezwa Jumamosi (Mei 28), Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.


Tayari Benchi la Ufundi limeshafanya maamuzi ya kujaza nafasi ya Kapombe kwa kumwita Lusajo Mwaikenda wa Azam FC.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger