Mchepuko Anatishia Nisipomhudumia Nitasaidiwa Majukumu na Wanaume wenzangu

 


Hii Ni baada ya kuangukiwa kitu kizito kutoka juu ya shelve na kuumia bega la kushoto na michubuko kadhaa shingoni. Hali Iliyonipelekea kulazwa kitandani kwa Siku 3 hospitali.


Sasa Siku ya 1 baada ya kufika hospitali na kupatiwa huduma ya kwanza,

Niliwapigia kuwafahamisha baadhi ya watu wangu wa karibu kua nmelazwa nmepata ajali na kuwarushia baadhi ya picha za jeraha langu, akiwemo Mchepuko wangu mamaJ.Nae Akaitikia na kunipa pole. Ikaisha.


Siku ya 3

mida ya saa 3 usiku Mchepuko Wangu mamaJ kanipigia anaulizia,

"Vipi mme wangu ushalala?"


Nikajibu, "sijalala"


Akasema "Usiku umeenda mme wangu, tunakula Nini?"


Nikajibu "Ndo nmemaliza kula wali na samaki Hapa"


Akasema"mi tangu mchana sijala uku"


Nikauliza "Kwann"


Akajibu "Si ujaniachia ela ya kula"


Nikauliza "kwani leo ujaenda kazin?"


Akajibu "nmeenda"


Nikauliza "kwani posho ya siku hamjapewa?"


Akajibu

"Tumepewa ndio, kwani tangu lini umeanza kuhusisha posho ya kazin kwangu na Ela yangu ya kula?"


Nikamwambia,

"Nakushangaa sana unaponiomba Ela ya kula wkt unajua kabisa nmelazwa na siendi kazini. Afu unanambia tangu mchana ujala wkt kazin najua unaposho ya siku. Hivi kabisa umekosa aibu, angalau ukajibana bana kwa Iyo posho unayopewa kazin kwako ukisubiri nipone ndo unambie huo upuuzi wako?"


Akasema,

"Inamaana Mimi kula kwangu Ni upuuzi?"


Nikamjibu,

"Ni upuuzi ndio, Kwasababu umelileta suala lako bila kuzingatia utu Wala mazingira niliyokuepo kwamba naumwa,nmelazwa na siendi kazini"


Akasema

"Inamaana wee ukiumwa,ukilazwa, inamaana sisi tusile?

Unataka kunambia hata MKEo mamaG uko nyumbani kwako Hali chakula kisa wewe umelazwa?"


Nikamjibu,

"Ebu ficha UPUMBAVU wako Basi, usitake kunikera"


Akasema,

"Inamaana Mimi KUOMBA chakula nmeshaanza kua KERO kwako sio?

Basi sawa, isiwe tabu basi. Sitakukera Tena babaG. Ujue sio kwamba nakung'ang'ania sana. Wanaume wako wengi sana wanaonililia wananitaka. wewe Kama huwezi kunihudumia,wapo wanaiweza kunihudumia. Sema tu Sina Ela,ili usidiwe majukumu yako."


Nikauliza, "unasemaje? Hebu rudia?"


Akasema

"nimesema Kama huna Ela, Sema TU sina ela ili usaidiwe majukumu yako na Wanaume wenzako"


Nikauliza

"Inamaana uko ndo ulikofikia mamaJ? Hivi Unanichukiliaje kwanza kunitamkia upuuz huo"


Akajibu,

"Nakuchukulia Kama mwanaume mbabaishaji, usiejua kutimiza wajibu wako kwa mwanamke wako, HAIWEZEKANI mimi unishindishe njaa siku mbili afu eti nikuchekee"


Nikamuuliza,

"Inamaana siku mbili sijakuachia Ela ya kula ndo zimetosha kuhitimisha mimi sitimizi wajibu wangu?

Hapo unapokaa Kodi unalipa wewe?

Kazini unakofanya kazi, unalipwa mshahara na posho, hiyo kazi umejipa wewe?

Hivi unafahamu ndani ya hizi siku 2 unazosema sijakupa Ela ya kula, afya yangu ilikuaje?

Inamaana afya yangu sio lolote Wala chochote kwako?

Hivi serious wewe Ni wakulalamika eti siku 2 zote umeshinda njaa kisa ujaachiwa Ela ya kula mezani?"


Nikaongezea

"Ujue wee mwanamke usitake kunipanda kichwani, wee Kama unatafuta sababu ya kuachana na Mimi au kucheat. Be straight and forward. Hata Kama unipendi au una ubinafs na roho mbaya, hebu jaribu kujistukia na kufunika kidogo Basi. Sio kuweka wazi hadharani namna Hii. Unatia aibu sana wee mwanamke"


Akasema, "utajua mwenyewe bhana" Kisha akakata Simu.


Sasa leo,

Ni siku ya pili tangu nmeruhusiwa kutoka hospitalini, Ni siku ya 3 Sasa tangu maongezi yale tuliyolumbana. Hajanipigia wala kunitumia sms yoyote kunijulia Hali naendeleaje afya yangu.


Na Mungu akijalia kesho nikiamka vizur naweza kuanza kwenda tena kazini.


Ila Nilichoazimia,

1. Sitamtafuta Tena kwenye Simu nione mwisho wake utakua Ni upi.


2. Sitompa Ela yoyote ya matumiz mpk nione mwisho wake utakua Ni upi.


3. Nitafatilia kimya kimya niwaone hao wanaume anaojitapa nao wanamtaka sana,wanajua wajibu wao na wako tayar kumhudumia na kunisaidia mimi majukumu.


3. Kama Ni kuachwa,

Kwa moyo msafi Niko tayar kuachwa kwa sababu anazosema yeye za kumshindisha njaa siku 2 bila kumpa Ela ya kula, na anajua nimelazwa naumwa.


NAWASILISHA


By DeepPond


______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad