Mchezaji Mtata Benard Morrison Kutangaza Timu Atakayocheza Msimu ujao

 


Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison ameweka wazi mpango wa kutangaza timu yake mpya atakayoitumikia msimu ujao wa 2022/23, baada ya kupewa mapumziko na Simba SC hadi mwishoni mwa msimu huu.


Morrison alipewa wasaa huo na Simba SC majuma mawili yaliyopita, huku ikifahamika mkataba wake na klabu hiyo ya Msimbazi utamalizika mwishoni mwa msimu huu 2021/22.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, kiungo huyo ameweka wazi mpango huo kwa kuandika ujumbe unasomeka “Tafadhali gusa link iliyopo kwenye bio yangu, jisajili kwenye channel yangu na subiri live video kwenye Youtube kujua kituo kinachofuata”.


Morrison alisajiliwa SC mwishoni mwa msimu wa 2019/20, baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi sita na Young Africans iliyomleta nchini wakati wa Dirisha Dogo msimu wa 2018/19.


Akiwa Simba SC ametwaa Ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’, Ngao ya Jamii na kufika hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad