Mgomo wa daladala Arusha, Polisi waonya wanaohamasishaArusha. Magari madogo ya abiria maarufu daladala katika Jiji la Arusha yamegoma kutoa huduma na kusababisha adha kkwa wasafiri katika Jiji hilo.

Wamiliki wa magari ya abiria wanaendesha mgomo kuanzia leo Mei 5, 2022 wakipinga kuzuiwa kupandisha nauli hadi ifikapo Mei 15 licha ya bei ya mafuta kupanda kuanzia Mei 3,2022.

Dereva wa daladala zinazofanya safari kati ya stendi ya magari madogo hadi eneo la kwa Mromboo, Jumanne Peter amesema wanataka nauli ipande kutoka 400 hadi 550.

"Hatuwezi kufanya kazi ya hasara bei mafuta upo juu sana leo dizeli inauzwa Sh3317 lita moja na bei za vitu vingi zimepanda"amsema


 
Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Mkoa Arusha na Kilimanjaro, Locken Adolf ameomba Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) kuruhusu bei kupanda sasa kwani tayari bei ya mafuta bei ipo juu.

"Mfano sasa gari za Moshi- Arusha tunapata Sh95,000 lakini mafuta pekee tunalipa Sh90,000 bado kuna malipo ya stendi hivyo sasa kila safari tunapata hasara ya wastani wa Sh20,000"amesema

Rehema Ninja amesema amelazimika kutumia Sh5000 kutoka kwa Mromboo hadi Stendi ya Arusha mjini kutokana na mgomo wa daladala.


Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Justin Masejo amewataka baadhi ya watu kuacha kuchochea mgomo na kufanya uhalifu.

"Tunawaonya ambao wanafanya uhalifu kipindi hiki, ulinzi umeimarishwa na watuhumiwa watakamatwa"amesema.

Aprili 30 mwaka huu Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) ilitangaza nauli mpya za mabasi ya mijini maarufu daladala na mabasi ya masafa marefu ambazo zitaanza kutumika baada ya siku 14.

Akitangaza kiwango hicho kipya cha nauli Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Gilliard Ngewe alisema mabasi ya mjini kuanzia Kilomita 0 hadi 10 nauli itakuwa Sh500 badala ya 400 na nauli ya Sh450 itakuwa ni 550.

"Kwa kilomita 30 nauli itakuwa 850 badala ya 750 na kwa kiliometa 35 nauli itakuwa 1000 na kwa huku kwa upande wa Kilometa 40 nauli itakuwa 1100" alisema Ngewe

Alisema kwa mabasi ya mkoani daraja la kawaida kwa kwa Kilometa 1 imeongezeka kwa asilimia 11 kutoka Sh 36 kwa kilometa moja hadi Sh41.

"Kwa daraja la kati imeongezeka kwa asilimia 6 abiria mmoja atalipa Sh56.88 kwa kilometa kutoka Sh53" alisema.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad