5/09/2022

Miriam Odemba "Ibrah Ndiye Mume Niliye Mchagua, Nimeridhika na Mahaba yake"


Mwanamitindo Miriam Odemba amesema kuwa Ibraah ndiye mume wa chaguo lake huku akitangaza kuridhika na mahaba yake.

Star huyo mwenye umri wa miaka 40 ameeleza kuwa tayari amezama kabisa kwenye mahaba ya Ibraah ambaye wamepishana kwa miaka 17.

"Nimemkolea Ibraah kwa sababu mtoto laini, mtoto safi, mwanaume asiye na maskendo na ndiye mume wangu mnipige mniue. Huku chuma, huku sumaku niwaibie siri kabisa kwa hili Miriam Odemba siambiliki kabisa kwisha yenu habari," Odemba amesema.

Ameendelea kwa kutaja sababu zake kutoka kimapenzi na msanii huyo wa Kondegang licha ya pengo kubwa kati ya umri wao.

Odemba amesema kuwa amevutiwa sana na sura ya Ibraah, mchezo wake wa kitandani na maisha yake rahisi yasiyozingirwa na drama nyingi.

"Hilo swala la kuhangaika na watu wazima wenzangu kama wengine wanavyosema kwa sasa kwangu lipo likizo na inatakiwa mjue kwamba ukubwa jalala mtu mzima ni kutafutiana lawama za kutoridhishana mahabani. Sasa ya nini yote hayo mimi sitaki lawama!" Miriam Odemba amesema.


HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger