Morrison Avunja Ukimya Sakata la Kufukuzwa SIMBA..Adai Barbara Ndio Hamtaki...Simu zake Hazipokelewi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Mchambuzi wa soka nchini, Saleh Ally 'Jembe' ametoa habari za ndani kabisa kuhusu mustakabali mzima wa mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Ghana Bernard Morrison na hatima yake ndani ya kikosi hicho chenye maskani yake mtaa wa Msimbazi, Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Saleh amedai alipata fursa ya kuongea na Bernard Morrison na moja ya kitu alichomhakikishia ni kwamba amechukua mizigo yake na tayari anaondoka kuelekea kwao Ghana kwani anaona kabisa kama haitajiki tena na klabu ya Simba.


Jembe anadai kwa maelezo ya mchezaji huyo kikwazo kikubwa na Mtendaji mkuu wa Klabu hiyo Barbara Gonzalez ambaye anadaiwa ndiye aliyetoa maelekezo ya Morrison kuondolewa katika kikosi cha wachezaji wa Simba, na ile hojaya kwamba Morrison ana matatizo ya kifamilia si ya kweli kwani Morrison mwenyewe amethibitisha kuwa hana matatizo yoyote yake ya kifamilia.


Kwa mujibu wa Bernard Morrison anadai kuwa amefanya jitihada nyingi za kuhakikisha kuwa anasaini mkataba mpya ikiwemo uwabembeleza baadhi ya viongozi ili abaki msimbazi lakini Mtendaji Mkuu Barbara amekuwa mwiba mkali wa kuzui hilo lisitokee na badala yake wakati mazungumzo yakiwa yanaendelea akapewa likizo ya lazima.


“Ameniambia mi naenda kutoa vitu vyangu vyote kwenye nyumba ya Simba kesho naondoka naenda nyumbani kama ntapata muda tutafanya Interview lakini kama nikikosa nikirudi tutafanya interview.”alinukuliwa Saleh Jembe akiongea kuhusu Morrison.


Bernard Morrison alitolewa kwenye kikosi cha Simba kinachoendelea kushiriki mashindano ya Ligi Kuu ya NBC kwa sababu ya kuwa ni ana matatizo ya kifamilia jambo linalomfanya kuwa nje ya uwanja hadi mwisho wa msimu huu.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad