Msemaji Simba Ahmed Ally Asema Ukweli Mchungu " Nisiwe Mnafiki Tunawaombea Mabaya Yanga"

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 


Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema wanaiombea mabaya Young Africans ili ipoteze michezo inayowakabili kabla ya msimu huu kufikia ukingoni.


Ahmed ametoa kauli hiyo baada ya Simba SC kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Kagera Sugar jana Jumatano (Mei 11), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.


Ahmed amesema: Pasina kuwa mnafiki niseme kwamba tunawaombea mabaya, alisema Afande Sele ‘Adui muombee njaa.”


Katika hatua nyingine Ahmed amesema baada ya kumalizana na Kagera Sugar, kikosi cha Simba SC kimeanza maandalizi ya mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Pamba FC, utakaopigwa Jumamosi (Mei 14) Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Tumemnyoa Kagera Sugar hapa Dar es salaam, tunamsubiri Pamba FC katika mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ naye tuje tumalizane naye, tuelekee hatua inayofuata. amesema Ahmed Ally


Mchezo huo ulipaswa kuchezwa mwezi April, lakini uliahirishwa kufutia Simba SC ilikua inakabiliwa na mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini


 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad