Mwanamuziki Kanye West Ashtakiwa na Askofu Mashtaka Haya


Mzimu wa madai unaendelea kumuandama Kanye West. Mtandao wa TMZ unaripoti.

Rappa huyo anaripotiwa kushtakiwa na Askofu David Paul Moten kutoka Texas kwa madai ya kuwa amesample moja kati ya audio ya mahubiri yake na kuitumia katika ngoma yake ya "Come To Life" inayopatikana kwenye album ya Donda bila ya ridhaa yake.

Askofu David Paul Moten pia amezishtaki , UMG, Def Jam pamoja na Good Music katika msala huo hivyo anadai fidia alipwe na pande zote hizo nne.

Katika nyaraka zilizodakwa na TMZ, Askofu Paul Moten anadai kuwa mahubiri yake yalitumika kwa muda wa sekunde 70 katika ngoma hiyo yenye dakika 5 na sekunde 10, ambayo ni zaidi ya asilimia 20 ya wimbo huo.

✍️: @omaryramsey

#SNSEnt
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad