Mwanamuziki P Diddy Afungua Label Mpya ya Muziki Love Records Kwa Ajili ya Muziki wa R&B Pekee

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPADiddy leo amezindua na kuitambulisha Label yake mpya ya muziki iitwayo “Love Records” ambayo maalum itasimamia na kufanya kazi na wasanii wa muziki wa R&B pekee. Label hiyo itafanya kazi chini ya ushirikiano na kampuni ya Motown Records.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Diddy alisema ana furaha kuitambulisha label hiyo ambayo itafanya kazi na wasanii wapya wa muziki wa R&B pamoja na watayarishaji wenye uwezo mkubwa. Kwa upande wake ameichukulia kama ukurasa mpya wa maisha yake ya muziki kwani pia ameahidi kurudi kwenye muziki na ataachia Album chini ya label yake hiyo.

Mwaka 1993 Diddy alianzisha label yake iitwayo “Bad Boy Records” na ilipata mafanikio makubwa ikifanya kazi na wakali wa dunia kama marehemu Notorious B.I.G, Faith Evans, 112, Mase, Cassie na wengine kibao.


 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad