5/28/2022

Mwanaume Aliyewaomba Madaktari Kumuokoa Hata Kama Akibaki Kichwa tu Baada ya Kupata Ajali Mbaya

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

Loren Schauers(20) toka Montana nchini Marekani aliiomba familia yake na madaktari waokoe maisha yake hata kama akibaki kichwa tu juu ya sahani

Mwaka 2019, Loren alikuwa mzima wa afya na viongo vyote. alikuwa anafanya kazi katika folklift ambayo akiwa pembezoni mwa daraja folklift hiyo ilimbonda vibaya sehemu ya chini ya mwili wake. Hospitali walimfanyia upasuaji kuondoa viongo vyote kuanzia kiunoni kushuka chini


Kwa mujibu wa Daily Star wakifanya nae mahojiano, madaktari wakiwa wanajadiliana na familia yake waruhusu kuwa inahitajika akatwe kabisa sehemu ya chini mwili wake kumnusuru ingawa matumaini ya kuishi sio makubwa, familia yake ikawa bado haina jibu la kutoa

lakini Kama miujiza Loren akaamka kutoka kwenye operesheni na kuomba madaktari wafanye chochote kumfanya aendelee kuishi hata Kama atabaki kichwa tu kwenye sahani


Aliondolewa vitu vyote kuanzia kwenye nyonga kushuka chini ikiwemo viungo vyake vya uzazi kuondolewa na sehemu ya mkono wa kulia iliyoharibika pia kuondolewa. Miaka miwili sasa imepita ameendelea kuishi

Licha ya kuondolewa viungo vya uzazi lakini jamaa huyo mwenye miaka 20 ana mke anayeitwa Sabia(23) ambaye anamsaidia kwa ukaribu mume wake huyo baada ya kupatwa na ajali iliyompa ulemavu wa kudumu


Loren na mkewe wameanzisha channel ya YouTube ambayo kwasasa ina subscribers zaidi ya laki 5 ambapo wanaonesha maisha yao

Sabia ameonekana kukerwa na baadhi ya maswali ya watu mitandaoni hasa wanaouliza wanafanyaje mapenzi wakiwa Kama wannado. Ambapo mke amesema kamwe hatokuja kujibu swali hilo kwakuwa hilo ni suala binafsi sana la ndani ya mtu au nyumba


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger