Mwenyekiti Simba SC amshangaa Bernard Morrison

 


Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC Murtaza Mangungu amemshangaa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison, kwa kushindwa kutimiza miadi waliyowekeana, baada ya klabu hiyo kumpumzisha hadi mwishoni mwa msimu huu.


Uongozi wa Simba SC mapema mwezi huu ulitangaza hadharani kumpa mapumziko Morrison hadi mwishoni mwa msimu huu, kufuatia matatizo yake binafsi, huku Mkataba wake ukielekea ukingoni.


Mangungu amesema Uongozi wa Simba SC ulikubaliana na Kiungo huyo mambo kadhaa, ili kumuwezesha kurudi nyumbani kwao Ghana kwa ajili ya kutatua matatizo yake, lakini cha kuchangaza Morrison alikatisha mawasiliano ghafla.


“Bernard Morrison aliomba kuondoka akashughulikie matatizo yake ya kifamilia, Sisi tulifanya kila kitu kuhusu safari yake ikiwa pamoja na kumkatia tiketi, Mpaka sasa hatujui alipo, simu hapokei, Kwa sababu Simba SC sio jela hatuwezi kuhangaika kumtafuta kujua alipo”


“Kama nyumbani kwao aliposema anakwenda ni Young Africans, basi atajua mwenyewe. Lakini viongozi wa klabu ya Young Africans watakuwa hawajitambui maana amewahangaisha sana” amesema Mangungu


Morrison anahusuishwa na mpango wa kusaini Young Africans, huku taarifa za baadhi ya vyombo vya habari zikidai tayari ameshamalizana na Uongozi wa klabu hiyo ili kukamilisha usajili wake huko Jangwani.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad