Nandy Apewa Tuzo na YouTube Kwa Kufanya Hili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Muimbaji nyota wa muziki wa bongofleva nchini, msanii @officialnandy amepewa tuzo na mtandao wa Youtube (Gold Plaque) kwa kufikisha wafuatiliaji (subscribers) Milioni 1 (1,000,000) kwenye channel yake.

Tuzo hiyo imekuwa ikitolewa kwa watoa maudhui kwenye mtandao wa Youtube ambao channel zao zinafikisha wafuatiliaji (subscribers) kuanzia 100,000 na kuendelea.

Nandy ambaye mwezi ujao anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake rappa Billnass, alijiunga na mtandao wa youtube Julai 5 mwaka 2016, anakuwa msanii wa pili wa kike nchini kufikisha Idadi hiyo kubwa ya wafuatiliaji (1M) kwenye mtandao huo.

Anayeongoza kuwa na (subscribers) wengi kwa wasanii wakike nchini ni Zuchu ambaye anawafuatiliaji (1.97M), watatu ni Rose Muhando (577K), wanne ni Christina Shusho (475K), na watano ni Vanessa Mdee (303K) ambaye kwasasa kajiweka kando na masuala ya muziki.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad