Netflix Yasitisha Kuonesha Filamu ya Meghan - PearlNetflix imesitisha mwendelezo wa filamu ya Pearl, iliyoandaliwa na Meghan Markle, katika harakati zake za kupunguza gharama.


Filamu hiyo ambayo ilitangazwa mwaka jana, ni moja ya miradi kadhaa iliyositishwa na gwiji wa kuonesha filamu.

Mwezi uliopita, Netflix ilibainisha kushuka kwa kasi ya waliojisajili na kutoa angalizo kuwa mamilioni zaidi ya watu wako tayari kuacha kutumia huduma hiyo.
Hiyo ilipunguza zaidi ya $50bn kutoka kwa thamani ya soko ya kampuni hiyo huku wataalam wakionya kuwa inakabiliwa na shida kurejea kwenye soko.
Archewell Productions, kampuni iliyoundwa na Duke na Duchess ya Sussex, ilitangaza mwaka jana kwamba Meghan atakuwa mtayarishaji mkuu wa Pearl.
Mfululizo wa filamu hiyo ulipangwa kuzingatia matukio ya msichana wa miaka 12, ambaye ameongozwa na wanawake wenye ushawishi kutoka kwa historia.
Licha ya kwamba Netflix ilithibitisha kuwa itaendelea kufanya kazi kwenye miradi kadhaa na Archewell Productions, pamoja na makala inayoitwa Heart of Invictus.
Filamu hiyo inayolenga wanariadha wanaoshindana na wanamichezo wakongwe waliojeruhiwa, tukio lililoanzishwa na Prince Harry, huko The Hague mnamo 2022.
Archewell Productions haikujibu mara moja ombi la BBC la maoni ya ufafanuzi zaidi.
Netflix pia ilisema kwamba imeamua kutoendelea kuonesha mfululizo wa filamu mbili za watoto zilizohuishwa za Dino Daycare na Boons and Curses.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad