Ni marufuku mtu yoyote kuuza jezi ya Ubingwa wa Yanga – Haji ManaraAfisa habari wa Miamba ya soka Afrika Mashariki na Kati, Mabingwa wa Kihistoria Ligi Kuu soka Tanzania Bara Young Africans Sports Club. Haji Manara ametoa katazo kwa baadhi ya watu ambao wenye nia ya kuuza jezi ya Ubingwa kwakua timu hiyo bado hazijazitoa.

Manara ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii ”Ni marufuku mtu yoyote kuuza jezi ya Ubingwa wa Yanga Coz Club bado haijazitoa. Jezi zetu zitatolewa na kuuzwa kwa utaratibu Maalum ambao Club na GSM watatwambia. Tunawasihi sana Washabiki wetu kutowanufaisha Wajanja wachache ilhali Club haifadiki. Yes: Yanga Bingwa lakini bado hatujatoa T-shirts wala Jezi za ubingwa, Soon tutawapa utaratibu.”

Yanga mpaka sasa amebakiza point tatu tu ili kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu baada ya kuukosa kwa muda mrefu wa zaidi ya miaka tatu, huku ikiwashuhudia watani zao Simba SC wakilitwaa mara nne mfululizo.

Imeandikwa na @fumo255
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad