Odemba "Polisi Itoe amri Kajala arudi kwa Harmonize"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwanamitindo maarufu na mtanzania anayeishi nchini Marekani Miriam Odemba ameliomba Jeshi la Polisi kuingilia mapenzi ya Harmonize kwa Kajala, kwa kutoa amri kwa Kajala kurudiana na Harmonize.

Odemba ameandika hayo katika mtandao wake wa Instagram, na yanajiri baada ya Harmonize kendelea kumlilia Mpenzi wake wa Zamani, Kajala, akiendelea kulipia mabango barabarani na kuonesha ni namna gani anampenda na anateseka na mapenzi mara baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Mzungu Briana.

Odemba pia amewaomba wasanii na wananchi ikiwa ni pamoja na mashabiki wa Harmonize kutoendelea kukaa kimya kuhusiana na sakata hilo kwa kuwa anaamini Msanii huyo maarufu ataweza kushuka kimuziki ikiwa ataendelea kubaki katika hali ya ‘stress’.

“Lengo likiwa ni kumuokoa Harmonize kutoka kwenye stress za mapenzi kwani akiendelea hivyo anaweza kushuka kimuziki,” aliandika Odemba.


Miriam Odemba kwa sasa anajulikana kama Shemeji wa Harmonize kutokana na kuonesha wazi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Msanii kutoka Konde Music, Ibraah.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad