Raila Odinga Amteua Martha Karua Kuwa Mgombea Mwenza Urais Kenya

Mgombea Urais nchini Kenya kupitia muungano wa Azimio Raila Odinga amemtangaza Martha Karua kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 9 mwaka huuAkizungumza katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta, Odinga amemsifu Karua kwa bidii na rekodi yake ya haki za binadamu.


"Baada ya kutafuta na kutafakari, pamoja na mashauriano, nimefikia uamuzi kwamba anayeshikilia nafasi hii lazima awe mwanamke," amesema Odinga 


Aidha katika hatua nyingine Odinga amemteua Stephen Kalonzo Musyoka kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri ili kumsaidia kuunda serikali ya Azimio.


Endapo Raila Odinga ataibuka mchindi katika uchaguzi huo itafanya Martha Karua kuwa mwanamke wa kwanza nchini Kenya kuwa Makamu wa Rais wa taifa hilo

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad