5/26/2022

Otile Brown Ameshindwa Kujizuia na Kufunguka Hadharani Jinsi Anavyomukubali Msanii Abby Chams

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

Staa wa Muziki Nchini Otile Brown ameshindwa kujizuia na kufunguka hadharani jinsi anavyomukubali Msanii wa Kike kutoka Tanzania Abby Chams. Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Otile ameonesha kuukubali uwezo wa Mrembo huyo kwa ku-share picha ya wimbo wa Rayvanny aliomshirikisha Abby Chams, STAY na kuandika ujumbe unaosomeka “Abby Chams Mashallah, Coming to Tanzania anytime Inshallah hopn to meet you queen ”

Ujumbe huo umewaaminisha mashabiki kuwa huenda wawili wana mpango wa kuja na wimbo wa pamoja hivi karibuni. Iwapo Otile Brown atafanikisha suala la kuachia wimbo wa pamoja na Abby Chams itakuwa ni kazi yake ya tatu kufanya na msanii wa Bongo fleva ikizingatiwa tayari ana Kolabo na Ali Kiba na Harmonize.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger