Pablo Acharuka Amtaja Chama, MorrisonSIMBA imecheza dakika 270 katika mechi tatu zilizopita na kufunga mabao mawili tu, jambo lililomfanya kocha Pablo Franco kucharuka na safu ya ushambuliaji, huku akiwataja Clatous Chama na Bernard Morrison aliowakosa juzi dhidi ya Namungo.

Katika mechi hizo zilizopita Simba ilitoka suluhu dhidi ya Polisi Tanzania na Yanga na juzi kutoka sare ya mabao 2-2 na Namungo, kitu kilichomfanya kocha huyo kuiangushia lawama safu ya ushambuliaji ya timu hiyo akidai imekuwa haijiamini na kukosa umakini.

Pablo alisema timu imekuwa ikitengeneza nafasi nyingi kwenye mechi zao za Ligi Kuu na hata ilivyokuwa kwenye michuano ya kimataifa, lakini umakini mdogo wa washambuliaji umekuwa ukiigharimu timu na kupata matokeo yasiyovutia.

Akizungumza na Mwanaspoti, Pablo alisema umakini wa washambuliaji wakiongozwa na Meddie Kagere, John Bocco na Chris Mugalu ndio changamoto kwake huku akisisitiza ameliona hilo kwa muda mrefu licha ya kupambana kuweka mambo sawa bila mafanikio. “Simba ina wachezaji wazuri na bora shida iliyopo ni kukosa mwendelezo wa ubora, leo wanaweza kukuonyesha kitu kikubwa, kesho mchezaji huyohuyo anaamka akiwa tofauti na vile ulivyomuandaa, kikubwa bado tuna nafasi tutaendelea kupambana ili kuhakikisha tunamaliza vizuri michezo iliyobaki,” alisema Pablo.


“Mchezo wetu dhidi ya Namungo tulikuwa na nafasi nzuri ya kuandika rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi ndani ya mechi moja kama washambuliaji wangu wangetumia kila nafasi walizotengeneza lakini imekuwa tofauti, tumejikuta tunaambulia sare ya 2-2.”

CHAMA, MORRISON

Kocha huyo kutoka Hispania alifafanua juu ya kukosekana kwa nyota wake wa kigeni, Clatous Chama na Bernard Morrison walioshindwa kumaliza dakika 90 katika dabi, alisema hawakusafiri na timu kwa sababu mbalimbali.

“Ndio maana nimesema mwendelezo wa ubora kwa wachezaji wa Simba haupo, nilikuwa nao na niliwaanzisha kwa pamoja dhidi ya Yanga lakini hawakufanya vizuri. Niliamini wangeongeza kitu dhidi ya Namungo ila walikosekana,” alisema Pablo.

“Chama ameachwa kwa vile anasumbuliwa na homa na kwa Morrison alikuwa na ishu zake binafsi. Japo siwezi kusema sare ya juzi imechangiwa kwa kukosekana kwao.”

Alisema huwa na matarajio makubwa na nyota wake, lakini wanamuangusha na ndio sababu inayomfanya ashindwe kuwa na kikosi cha kwanza kutokana na baadhi kukosekana kila mara.

“Sina kikosi cha kwanza kwasababu wachezaji hawana muendelezo mzuri wa ubora wao siwezi nikamtumia mchezaji ambaye ameshindwa kunionyesha kitu kwenye mazoezi eti kwani sababu amefanya vizuri mchezo uliopita.” alisema.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad