Panya Road 23 wadakwa, wadai walifanya matukio kulipa kisasi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



KAMANDA wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro, amesema wanawashikilia watuhumiwa 23 kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha (Panya Road), ambapo baadhi yao walikiri kufanya vitendo hivyo kwa ajili ya kulipa kisasi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kamanda Muliro ametoa taaria hiyo leo Alhamisi, tarehe 12 Aprili 2022, jijini Dar es Salaam, akielezea mafanikio ya operesheni endelevu ya kusaka vijana wadogo wanaovunja nyumba, kujeruhi wananchi na kuiba mali, iliyoanza tarehe 27 Aprili mwaka huu.

“Kufikia tarehe 11 Mei 2022, tayari wamekamatwaa watuhumiwa 23 kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya unyanganyi wa kutumia silaha mapanga na visu, kuvunja nyumba usiku, kujeruhi na kuiba vitu mbalimbali hasa maeneo ya Kitunda, Mwanagati Ilala na Kinondoni maeneo ya Kunduchi Mtongani na Tegeta,” amesema Kamanda Muliro.

Kamanda Muliro amesema “baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa walifanya tukio la unyang’anyi tarehe 10 Mei 2022, huku wakidai kulipa kisasi kwa baadhi ya watu wa maeneo hayo baada ya mtuhumiwa mwenzao kufariki kwa kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali kwa kujihusisha na wizi.”


 
Kamanda Muliro amesema kuwa, watuhumiwa hao waliokamatwa wana umri kati ya 13 hadi 24 na kuwa katika mahojiano nao, Jeshi la Polisi limebaini baadhi yao hawakumaliza shule ya msingi kwa utoro na sababu mbalimbali.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad