5/02/2022

"Panya ROAD Tuliowakamata ni Darasa la 5" - Polisi Wafunguka

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPAJeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema hadi sasa linawashikilia vijana sita (6), ambao ni Panya road, waliohusika na uvamizi maeneo ya Kunduchi Mtongani kwa ajili ya mahojiano ili waeleze wenzao wako wapi, kwanini wanafanya matukio hayo na wakipora vitu wanapeleka wapi.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Mei 2, 2022, na Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo Jumanne Muliro, mara baada ya usiku wa kuamkia leo vijana hao kujeruhi kwa mapanga watu 19, katika mtaaa wa Mtongani, Kata ya Kunduchi.

"Baadhi ya vijana tuliowakamata waliacha shule darasa la tano, wengine wanavuta bangi wanaseman kabla ya kufanya matukio lazima wawe kwenye mazingira ambayo yanaweza kuwapa ujasiri wa kufanya matukio mabaya ndiyo maana mtu anaporwa simu kwa kukatwa panga," amesema Kamanda Muliro

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger