Panya Road Wajeruhi 19 Dar es SalaamVijana wanaodhaniwa kuwa ni Panya road wamewakata mapanga watu 19 katika mtaaa wa Mtongani, Kata ya Kunduchi mkoani Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo Mei 2, 2022.
Tukio hilo limetokea masaa kadhaa tu tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, alipotoa onyo kwa vikundi hivyo kuachana na tabia hiyo, wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani iliyofanyika mkoani Dodoma.

Wakizungumza hii leo na East Africa TV mmoja wa majeruhi hao amesema kwamba, vijana hao walikimbilia ndoo ya pesa, huku wakimuwahi kwa kumkata mikono yake ili akose namna ya kupambana nao.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad