5/03/2022

Papa Asema Amejitolea Kusafiri Hadi Urusi Kukutana na PutinPapa Francis anasema amejitolea kusafiri hadi Moscow kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin ili kujadili kuhusu vita nchini Ukraine, lakini bado hajapata majibu


Papa aliliambia gazeti la Italia la Corriere della Sera kwamba alituma ujumbe kwa Kremlin siku 20 baada ya uvamizi wa Urusi, kupitia mwanadiplomasia mkuu wa Vatican.Ni mara ya kwanza kwa Papa kuitaja Urusi au kumtaja hadharani Putin tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine zaidi ya miezi miwili iliyopita.Papa pia alisema hivi karibuni aliwasiliana kupitia simu ya zoom ya dakika 40 na mkuu wa Kanisa la Orthodox la Urusi, Baba Mkuu Kirill anayeunga mkono vita, na alitumia dakika 20 za kwanza za simu hiyo kuelezea uhalali wake, aliambia gazeti hilo.Baba mkuu hawezi kujigeuza kuwa kijana wa madhabahu ya Putin, Papa alisema

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger