Raia wa Afrika Kusini afariki hotelini Tanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Raia wa Afrika kusini ambaye ni mhandisi mshauri katika mradi wa Bomba la mafuta ghafi kutoka Nchini Uganda-Tanga upande wa Tanga amekutwa amefariki katika chumba cha hoteli aliyokuwa amepanga kwa muda wa mwezi mmoja na nusu.

Raia wa Afrika Kusini aliyetambulika kwa jina la Abraham Jacobus amefariki Dunia katika chumba cha Hoteli ya (Tanga beach) jijini Tanga alipokuwa amepanga

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na  Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga  David Chidingi ni kuwa mtaalamu hiyo alifariki usiku wa kuamkia leo jumapili.

Mwili umehifadhiwa katika hopsitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga  Bombo.

Imeelezwa kuwa Abrahamu ana takribani mwezi mmoja na nusu akiishi katika hoteli hiyo na kwamba umauti umempata usiku wa kuamkia leo akiwa peke yake chumbani kwake.

Raia huyo wa Afrika kusini mpaka umauti unamkuta alikuwa anafanya kazi katika mradi wa bomba la mafuta kwa upande wa Tanga kama Mhandisi Mshauri.

" Dereva wake wakati alipomfuata kwa lengo la kumchukua kuelekea kazini  alimpigia simu kwa muda mrefu haikupokelewa na ndio  akatoa taarifa kwa uongozi wa hoteli na wakafungua na kumkuta amefariki na wakatoa taarifa polisi " amebainisha Kaimu Kamanda Chidingi.

Amesema uchunguzi wa awali umebaini  alikuwa na tatizo la athma na kwamba mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bombo kwa uchunguzi zaidi.

" Marehemu ni raia wakigeni hivyo kuna taratibu ili kufanya uchunguzi wa kina na kubaini hasa chanzo cha kifo chake ".amesema Kaimu kamanda huyo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad