5/23/2022

Raia wa Denmark ahukumiwa kunyongwa Nigeria kwa kumuua mkewe na mtoto

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Raia mmoja wa Denmark, Peter Nielsen amehukumiwa kifo nchini Nigeria baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mkewe na mtoto wao wa kike wa miaka mitatu.

Mahakama mjini Lagos imesema mwendesha mashtaka amewasilisha ushahidi wa kutosha kumtia hatiani mtu huyo ambaye amehukumiwa kunyongwa.

Mshtakiwa alikana kuhusika na mauaji hayo wakati kesi zikiendelea mahakamani. Mauaji hayo yalifanyika mnamo Aprili 5, mwaka 2018 katika nyumba ya wanandoa hao katika kitongoji tajiri cha Banana Island cha Lagos.

Kesi hiyo iliibua hisia ya umma, haswa kutoka kwa makundi ya kutetea haki za wanawake.


 
Hukumu ya kifo kwa kunyongwa ndio adhabu kuu kwa kosa la mauaji huko Nigeria, nchi ya Afrika Magharibi yenye watu milioni 212.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger