5/21/2022

Rais amuapisha Mwalimu aliyemfundisha form 2 na 3

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, leo amemuapisha Mwalimu aliyewahi kumfundisha masomo ya Kiingereza na Hesababu akiwa kidato cha pili na cha tatu kuwa Kamishna wa Tume wa Utumishi wa Umma.

Akizungumza hii leo Mei 21, 2022, mara baada ya kumuapisha, Rais Samia amesema kwamba ilikuwa ni ngumu sana kwa upande wake kumuapishwaa Mwalimu wake huyo.

"Leo nimepata kazi kidogo kumuapisha Mwalimu wangu Bi Khadija, huyu bibi vyovyote alivyo mfupi, mdogo ni mwalimu wangu wa Hesabu na Kiingereza Form Two na Form Three," amesema Rais Samia  

Aidha Rais Samia ameongeza kuwa, "Wale wa umri kama kina Bi Khadija, wakokoteni hivyo hivyo twende nao lakini ninajua akili iko vizuri, mimi kanifundisha akiwa kijana mdogo na nilikuwa nathubutu kusimama na kumuiga darasana nikijua anaingia basi nakwenda kwenye blackboard na-act exactly alivyokuwa akifanya napengine labda ndiyo maana nimekuwa hivi,".


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger