Rais Samia Aliandikia Bunge Barua


Rais Samia Suluhu Hassan, ameliandikia Bunge barua ya salamu za shukrani kuwashukuru wabunge kwa kujadili na kutoa azimio la kumpongeza baada ya kupata tuzo ya Babacar Ndiaye nchini Ghana, ambayo hupatiwa Rais wa nchi za Afrika zinazofanya vizuri kwenye miundombinu ya barabara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Barua hiyo imesomwa leo Mei 30, 2022, na Spika wa Bunge hilo Dkt. Tulia Ackson

"Kwa kipekee kabisa tuzo hiyo ni ya wabunge kwa kutambua mchango wenu katika kusimamia miradi, matumizi sahihi ya fedha za miradi na kupitisha na kusimamia bajeti ya serikali hivyo ninaomba Watanzania wote wafurahie tuzo huku tukiendelea kusimamia, kulinda na kuitunza miundombinu yetu," imeeleza sehemu ya barua ya Rais Samia kwa Bunge.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad