Rais Samia Atajwa Katika Orodha ya Watu 100 Wenye Ushawishi Mkubwa Duniani


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametajwa katika orodha ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani, kwa mujibu wa Jarida la TIME 100. Rais Samia ametajwa katika orodha hii kutokana na uongozi wake wa kusisimua tangu alipoingia madarakani Machi 2021.

Ameungana na Marais kutoka nchi nyingine katika orodha hiyo wakiwemo Volodymir Zelenskyy wa Ukraine, Xi Jinping wa China, Vladimir Putini wa Urusi na Joe Biden wa Marekani. Hii inakua mara ya pili kwa Rais Samia Suluhu kutajwa kwenye orodha za majarida makubwa duniani, Disemba mwaka 2021 alitajwa na Forbes kwenye orodha ya wanawake 100 wenye nguvu duniani.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad