Rais Samia Kufanya ziara ya Siku Mbili Uganda

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kiserikali ya siku mbili nchini Uganda kuanzia leo Jumanne Mei 10 -11, 2022, kwa mualiko wa Rais wa nchi hiyo, Yowei Museveni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa madhumuni ya ziara hiyo ni kuimarisha na kudumisha zaidi historia iliyopo na mahusiano ya kidiplomasia pamoja na ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili.

Imeeleza kuwa katika ziara hiyo, wanatarajiwa kujadili kuhusu masuala ya nishati, biashara, usafiri, maendeleo ya miundombinu pamoja na sekta za afya.

“Hii itakua ni ziara ya kwanza ya kiserikali nchini kufanywa na Rais Samia tangu Serikali ya Awamu ya Sita iingie madarakani mwezi Machi 2021” imeeleza taarifa hiyo.

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad