Rais Samia "Ukinikuna Vizuri Nitakukuna na Kukupapasa"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka waandishi wa habari nchini kuzingatia sheria na kufanya kazi kwa uungwana kwani wakimkorofisha hatowaacha. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Pia amewataka kuandika habari za kutunza na kuheshimu mila na desturi za kiafrika.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 3 Mei, 2022 jijini Arusha katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani.

Maadhimisho hayo yalikuwa na kauli mbiu isemayo “Uhuru wa vyombo vya habari na changamoto za kidijitali”.


Akitumia misemo mbalimbali ya Kiswahili iliyowaacha hoi mamia ya waandishi wa habari na wadau wa sekta hiyo waliohudhuria maadhimisho hayo, Rais Samia amesema Serikali inatumia busara kutekeleza sheria ya masuala ya habari.

“Busara tunayotumia ni ule msemo wa kizungu, ‘scratch my back I’ll scratch yours’, ukinikuna vizuri mimi nitakukuna na kukupapasa huku nakupuliza, lakini ukinipara nitakuparura… tuende tufanye kazi kwa uungwana, kuelewana, ukinikuna nitakupapasa, lakini ukinipara nitakuparura, sheria zio palepale,” amesema.

Aidha, amesema miaka ya nyuma ilikuwa ngumu kwake kukaa na kusalimiana na viongozi wa majukwaa ya waandishi wa habari kama Deodatusi Balile lakini sasa hakuna haja ya kugombana tena.


“Niulize jambo moja… tunagombana kitu gani, fikira na mueleko wote ni Watanzania, tunajenga nyumba hiyohiyo, tunagombana kitu gani! Kama kuna tofauti tukae tuzungumze tuendeleze nchi yetu. Hakuna kugombana… why tugombane! hii ndio raha ya mwanamke anakuwa anaongoza familia,” amesema.

Amesema zipo mila potofu za kupigiwa kelele na kuwaelimisha wananchi lakini zile mila nzuri zisifiwe.

“Wakati sisi tunaponda mila zetu wenzetu wanazitaka hizi hizi, lakini sio za kwao hawawezi kufanya kama sisi ndio maana unakuta mwanamke mzuri katoka nje kaolewa na mwanaume wa kiafrika ukimwangalia unasema eeh! Vipo anavyovifuata huku… ni mila, desturi na namna ya kuishi,” amesema.

Aidha, amewataka waandishi wa habari kuanzika mazuri ya kiafrika na kuacha kuwa mawakala wa vyombo vya habari vya nchi tajiri kwa kuandika mabaya ya Afrika na kutia chumvi.


Amesema hatua hiyo ya kuandika mabaya pekee ya Afrika ni sawa na kujivua nguo.

“Watanzania, mnaenda kujivua nguo na kuwaambia wengine kuwa huku hakuna demokrasia, kuna udikteta, sijui huyu mama kafanyaje. Jivunieni kilicho chenu, tukuzeni kilicho chenu. Hata akitokea nani akawaandika hatakiandika vizuri mtakavyoandika wenyewe.

“Kingine mnalindwa, serikali inawalinda, mashirika mbalimbali lakini hakuna mlinzi mzuri kama wewe mwenyewe, tazama unalofanya pima nikifika mpaka hapa inatosha, yule mama nitamkorofisha na mimi sitokuacha,” amesema.

Aidha, alimuagiza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kukaa na vyombo vyake na kupitia maudhui yanayorushwa mitandaoni kuhusu watoto ili kukinga mila na desturi za Taifa.


“Leo kuna katuni zilizopo mitandaoni mwanaume kwa mwanaume wanabusiana, mwanamke kwa mwanamke wanashikana… hatuzidhibiti na siku hizi mtoto akizaliwa leo ukimuwekea ipad anafungua anatizama kila kitu. Kafundishwa na nani hujui, nadhani ukuu wa Mungu kawaumba hivyo,” amesema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad