Rais Samia "Safari zangu zina Manufaa Fanyeni Tasmini"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka wanaokosoa safari zake nje ya nchi, wafanye tathmini ya safari hizo kabla ya kukosoa kwa kuwa zimekuwa na manufaa kwa nchi.

Rais Samia ameyasema hayo leo katika mahojiano maalumu na Tido Mhando wa Kituo cha Televisheni cha Azam, Ikulu Chamwino, Dodoma.

Amesema alipoapishwa kuwa Rais, safari yake ya kwanza aliifanya nchini Kenya, ambako kwa kushirikiana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, walifanikiwa kuondoa vikwazo 64 vya kibiashara vilivyokuwepo kati ya Tanzania na Kenya.

Amesema kulikuwa na sintofahamu ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili, ikiwemo malori kuzuiwa mipakani kwa muda mrefu, kuchomwa kwa vifaranga vya kuku na mahindi kuzuiwa kutokana na madai ya kuwa na sumukuvu.


“Lakini nilipokwenda tukazungumza, tukaondosha vikwazo vile vyote, sasa hivi biashara kati ya Tanzania na Kenya imekua maradufu, na imekuwa zaidi kwa upande wetu,”alisema Rais Samia.

Baada ya kutoka Kenya alisema alikwenda nchini Uganda, ambako nako kulikuwa na shida kidogo kwenye mradi wa bomba la mafuta na tatizo hilo liliondolewa na mradi unaendelea na kisha akaenda Umoja wa Ulaya, ambako nako kulikuwa na miradi ya Tanzania iliyokwama, lakini sasa inaenda vizuri.

Alisema safari zake anakwenda na wafanyabiashara na kuwakutanisha na wafanyabiashara wenzao, ambako kumesainiwa mikataba kadhaa ya ushirikiano.


“Juzi tumerudi kutoka Marekani, tumesaini mikataba ambayo kama itatekelezwa kila mkataba karibu Sh trilioni 11. Wafanye tathmini enzi hizo hatuendi biasahara ilikuwaje ndani na sasa tunakwenda biashara ikoje,”alisema Rais Samia
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad