Rais wa Tanzania Samia Suluhu Apokea Tuzo ya Heshima ya Babacar Nchini Ghana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa tuzo yake ya heshima ya Babacar Ndiaye nchini Ghana
RAIS Samia anapokea tuzo ya mwaka 2022 ya Babacar Ndiaye kwa mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji ambayo hutolewa kwa Mkuu wa nchi iliyofanya vizuri.

Baada ya kupokea tuzo hiyo Rais Samia amesema anajisikia faraja kwa kuwa Rais wa Kwanza Mwanamke Barani Afrika kupokea tuzo hiyo kwani ni heshima kwake na heshima kwa kile anachokifanya katika nchi yake.

Rais Samia amesema suala la utekelezaji wa miundombinu ni mchakato endelevu ambao umeanza tangu awamu ya kwanza ya muasisi wa Taifa la Tanzania Hayati Julius Nyerere lakini lilishika hatamu zaidi katika awamu ya nne ya utawala wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambao uliendelea hadi kufikia katia awamu yake na ni mengi yamefanyika kuhusu suala la miundombinu.

Ameongeza kwa kusema ili Bara la Afrika liweze kujikomboa kiuchumia miundombinu ni jambo mtambuka na lazima lipewe kipaumbele ili liwweze kusaidia kukuza uchumi wa Afrika.

Rais Samia amebainisha kuwa 60% ya ardhi iliyopo Afrika inafaa kwa kilimo achilia mbali rasilimali nyingine zilizopo kama vle madini pamoja na utalii vyote hivi ili viweze kuwa na tija basi miundombinu mizuri lazima iwepo.

Kwa upande mwingine Rais Samia ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika AFDB kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Tanzania katika kuboresha miundombinu nchini, akisistiza kuwa anajisikia mwenye faraja kubwa kwa kufanikiwa kukamilisha baadhi ya miradi mikubwa ya miundombinu ndani ya muda mfupi wa utawala wake.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad