Rasmi Sasa Huyu Hapa Ndio Mwamba Anayemiliki Timu ya Chelsea


Todd Boehly na washirika wake wamemilikishwa rasmi klabu ya chelsea baada ya kukamilisha hatua zote ambazo serikali na bodi ya ligi waliziweka ili kuweza kuinunua klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.

Makabidhiano yamekamilishwa na kumilikishwa rasmi na pia Todd Boehly alitoa neno kupitia tovuti ya klabu ya Chelsea.

“Ni heshima kuwa wamiliki wapya wa Chelsea Football Club. Tupo hapa kwa asilimia 100, kila dakika ya mchezo.” alisema Todd Boehly.

“Maono yetu kama wamiliki yako wazi, tunataka kuwafanya mashabiki wajivunie. Huku tukijikita kwenye maendeleo ya kikosi cha vijana na kuleta vipaji bora, mipango yetu ya vitendo ni kuwekeza kwenye klabu kwa muda mrefu na kutengeneza historia ya mafaniko isiyofutika kwenye klabu ya Chelsea.”

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad