5/05/2022

Rihanna Ajengewa Sanamu Marekani Akiwa Mja Mzito


Makavazi ya Metropolitan Museum of Arts au ukipenda Met huko Manhattan New York nchini Marekani imeunda na kuonyesha sanamu ya mwanamuziki na mfanyibiashara Robyn Rihanna Fenty maarufu kama Rihanna.

Sanamu hiyo inamuonyesha Rihanna alivyo hivi sasa akiwa mjamzito. Mzaliwa huyo wa Barbados alifurahiya heshima aliyotunukiwa na makavazi hayo kwa kupost video ya sanamu hiyo kwenye ukurass wake wa Instagram.

“Nilishinda wote kwenye Met gala nikiwa sanamu! Ni nini cha thamani kushinda hicho?” aliandika Rihanna huku akishukuru makavazi ya Met na Jarida la Vogue.

Sanamu hiyo ilionyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye hafla ya mwaka huu ya Met Gala ambayo huandaliwa na jarida la Vogue iliyofanyika Jumatatu katika makavazi ya Met. Met Gala ni hafla ya maonyesho ya mitindo ya mavazi ambayo huandaliwa Jumatatu ya kwanza ya mwezi Mei kila mwaka kwa ajili ya kuchangisha fedha za kufadhili makavazi ya Met. Inachukuliwa kuwa hafla kubwa zaidi ya maonyesho ya mitindo ya mavazi ulimwenguni na watu wote maarufu hutamani sana kuwepo.

Aidha, Rihanna hakuhudhuria hafla ya mwaka huu labda kwa sababu ya ujauzito na kukaribia kupata salama na kilichosababisha aenziwe ni uwezo wake wa kuongoza njia katika mitindo ya mavazi hata wakati huu ambapo yeye ni mjamzito.

✍️: @omaryramsey

#SNSEnt

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger