Rose amrithi Askofu Getrude RwakatareROSE Mgetta ambaye amesimikwa rasmi kuwa Askofu Mkuu wa Makanisa ya Mlima wa Moto Mikocheni kuchukua nafasi ya Mwasisi wa Kanisa hilo, Askofu Getrude Rwakatare amepongeza kazi kubwa zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Askofu Mkuu mteule wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni, Rose Mgetta akiongoza maandamano ya kwenda kumsimika kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Mikocheni jijini Dar es Salaam jana. Askofu Mgetta anachukua nafasi ya Mwanzilishi wa Kanisa hilo hayati Dk. Getrude Rwakatare aliyefariki mwaka 2020. (PICHA MIRAJI MSALA)
Dk. Rwakatare ambaye alianzisha Kanisa hilo mwaka 1993 alifariki dunia mwaka 2020 na tangu wakati huo Askofu Rose amekuwa akikaimu nafasi yake hadi Jumamosi Aprili 23,2022 aliposimikwa rasmi.

Ibada ya kumsimika Rose ilindeshwa na Askofu wa Makanisa ya ELIM Pentecoste Tanzania, Peter Konki kwenye Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na waumini wa kanisa hilo na wageni mbalimbali.

Akizungumza mara baada ya kusimikwa rasmi, Askofu Rose aliiushukuru uongozi mzima wa Kanisa hilo kwa kuamini kwamba anaweza kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi na kuamua kumsimika rasmi kumrithi Dk. Rwakatare.

Alisema wanawake wanaweza kufanya mambo makubwa wakipewa nafasi tofauti na fikra za baadhi ya watu waliokuwa hawaamini kwamba mwanamke anaweza kuwa kiongozi kwenye nafasi kubwa na kufanikiwa.


 

“Rais Samia Suluhu Hassan wakati anaingia madarakani baadhi ya watu walikuwa na hofu kwamba huenda asimudu nafasi hiyo lakini sote ni mashuhuda wa namna alivyomudu majukumu yake na nchi inakwenda vizuri sana,” alisema Askofu Rose

Alisema amekaimu nafasi hiyo kwa miaka miwili tangu kifo cha mwasisi wa kanisa hilo, Dk. Getrude Rwakatare mwaka 2000 na baada ya kufanya kazi nzuri ya utumishi waumini na uongozi wa kanisa umeona kwamba anafaa.

Aliwaomba Watanzania kushikamana na kuendelea kuishi kwa amani na upendo na kwamba viongozi wa dini kwa upande wao waendelee kutimiza wajibu wao wakuombea amani na kuwaombea viongozi wa nchi.


 “Mwasisi wa Kanisa hili Dk. Rwakatare alinilea vizuri sana na nilikuwa chini yake kwa muda mrefu ni mtu alipenda kuwainuia wanawake na mmoja wa wanawake aliowainua ni mimi hivyo nawaahidi waumini wa kanisa kazi iliyotukuka,” alisema Askofu Rose


Askofu mpya wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, ROSE Mgetta akiwa amezungukwa na maaskofu kwenye ibada ya kusimikwa rasmi kuwa Askofu Mkuu wa Makanisa ya Mlima wa Moto Mikocheni B kuchukua nafasi ya Mwasisi wa Kanisa hilo, Askofu Getrude Rwakatare.
Kwa upande wake, mtoto wa kwanza wa Dk. Rwakatare, Dk. Rose alisema Askofu huyo ana uzoefu wa kutosha kwani alifanyakazi kwa karibu sana na mwasisi wa kanisa hilo kwa muda mrefu akiwa msaidizi wake wa karibu.

“Sisi tumeona huyu ndiye anaimudu kazi hii kwasababu ameifanya kwa muda mferu akiwa na mama yetu na waumini wameahidi kuendelea kumpa ushirikiano kwasababu wanamwamini na wamekuwa naye siku zote,”: alisema

Alisema wanawake wanaweza kufanya mambo makubwa wanapopewa nafasi hivyo ni dhahiri Rose ataendeleza kanisa hilo kama ambavyo lilikuwa limesimama wakati wa uhai wa mwasisi wa Kanisa hilo Dk. Rwakatare.


 
Dk. Rose alisema waumini wa kanisa hilo wataendelea kuliombea taifa lizidi kuwa na amani wakati wote na aliwaomba watanzania waendelee kushikamana na kuishi kwa upendo ili kuhakikisha mshikamano uliopo unakuwa endelevu kwa ustawi wa taifa kwa ujumla.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad