5/04/2022

Ruvu Shooting Yaibana Mbavu Yanga, Mayele Ashindwa Kutetema TenaKLABU ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani imefanikiwa kuambulia alama moja mbele ya vinara wa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Klabu ya Yanga katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

 

Katika pambano hilo mshambuliaji hatari na kinara wa mabao Fiston Mayele alifanikiwa kugongesha mwamba wa lango mara mbili katika matukio tofauti huku akiwekwa chini ya ulinzi madhubuti na walinzi wa Ruvu Shooting.

 

Katika mchezo huo Ruvu Shooting imefikisha jumla ya alama 22 ikibaki katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi huku vinara Yanga wao wakifikisha jumla ya alama 56 na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo.


Mshambuliaji wa Yanga na Kinara wa mabao wa Ligi Kuu ya NBC Fiston Mayele

Mchezaji wa Ruvu Shooting Rashid Juma aliambulia kadi nyekundu kutoka na utovu wa nidhamu

Ruvushooting ipo katika harakati za kupambana kujiepusha na hatari ya kushuka daraja msimu huu kutokana na kutokuwa na matokeo mazuri kwenye baadhi ya michezo yake ya hivi karibuni

 

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger