Sababu Zilizopelekea Sabaya Kuachiwa Huru

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Arusha. Vilio vya furaha kwa ndugu ,jamaa na marafiki wa aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili leo vimetawala ndani na nje ya Mahakama Kuu baada ya Jaji Sedekiya Kisanya kuwaachia huru katika hukumu yake iliyochukua saa moja.

Katika hukumu iliyosomwa leo Mei 6,2022, Sabaya na wenzake wawili, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, walijikuta wakiwa huru baada ya jaji huyo kuona kasoro katika mwenendo wa kesi, hati ya mashtaka na mashahidi kutofautiana.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Kisanya alichambua hoja 14 za warufani na kusema kuwa hati ya mashitaka inatofautiana na ushahidi uliotolewa mahakamani hasa kuhusu kiasi cha fedha kilichoibiwa na vitu vingine.

Jaji Kisanya amesema angeweza kuagiza shauri hilo lirudiwe upya hasa kutokana na mapungufu ya kisheria, lakini ushahidi hauwezi kutofautiana na kilichozungumzwa mahakamani hivyo uamuzi ni kuwaachia huru wakata rufaa.


Katika hati ya mashitaka ilielezwa fedha zilizoibiwa ni Sh2,769,000, lakini mashahidi walieleza kuwa kiasi tofauti kilichoibwa na vitu vingine kama mashine ya risiti za kielekroni (EFD) na sarafu.

Amesema katika ushahidi imeelezwa watuhumiwa walichukuwa simu na fedha lakini katika mashitaka mashitaka haikuelezwa fedha kuibiwa.

Jaji amesema katika shauri hilo ilielezwa kulikuwa na kamera za CCTV, lakini hazikutolewa mahakamani licha ya mshitakiwa wa pili na tatu kueleza hawakuwepo kwenye tukio hilo katika duka la Mohamed Saad.

Mawakili wa Sabaya wapongeza uamuzi

Akizungumza nje ya mahakama baada ya rufaa hiyo, Wakili Mosse Mahuna amesema wanaishukuru mahakama kwa kutenda haki na kukubaliana na hoja zao rufaa.

Amesema hoja ambazo walikuwa wanazilalamikia waliziwasilisha hata wakati wa kesi ya msingi, ikiwa ni pamoja na mapungufu ya hati ya mashitaka na mwenendo wa kesi kuwa na mapungufu.

Sabaya na Silvester bado wana kesi ya uhujumu uchumi hivyo watarudishwa mahakamani, lakini Daniel Mbura yupo huru na wana imani baada ya kukamilisha taratibu za magereza ataachiwa leo.

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
 1. That’s a great article! The neatly organized content is good to see. Can I quote a blog and write it on my blog? My blog has a variety of communities including these articles. Would you like to visit me later? 토토

  ReplyDelete
 2. It was a very good post indeed. I thoroughly enjoyed reading it in my lunch time. Will surely come and visit this blog more often. Thanks for sharing. 경마사이트

  ReplyDelete
 3. That was an excellent article. You made some great points and I am grateful for for your information! Take care! 카지노사이트

  ReplyDelete
 4. I’ve seen articles on these topics a few times, but I think your writing is the cleanest I’ve ever seen. I would like to refer to your article on my blog and write it. 사설토토

  ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad