5/25/2022

Samia: Kuwa mwanamke kulinifanya nisiaminiwe Urais

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Samia: Kuwa mwanamke kulinifanya nisiaminiwe Urais
RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema changamoto ya kwanza aliyokutana nayo alipoingia madarakani ni kutoaminiwa kutokana na uwanamke wake.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Accra Ghana, katika meza ya majadiliano ya viongozi mbalimbali kitaifa wa Afrika, katika mkutano ulioandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB).

Rais Samia amesema: “Changamoto ya kwanza niliyokumbana nayo ni watu wa Tanzania kutoniamini, walitilia shaka kama nilikuwa na sifa ya kuongoza, wakati nilipochukua hatamu kwa sababu ni mwanamke.

“ Wengine hawakuamini kuwa mwanamke anaweza kuwa Rais bora, hawakuamini kuwa naweza kuendesha nchi, lakini ndani ya mwaka mmoja nimewaonesha kuwa mwanamke anaweza na mwanamke hawezi kufeli,” amesema Rais Samia na kuongeza:


 
“Kwa mwaka mmoja nimeonesha nguvu ya mwanamke,” kauli ambayo imeonesha kuwakuna Marais wengine na kupiga makofi ya kumshangilia.

“Nimeendesha nchi kama alivyokuwa anaendesha mtangaulizi wangu na nimefanya mengi mazuri  zaidi,” amesisitiza.

Rais Samia alichukua nafasi ya hayati Dk. John Magufuli aliyefariki Machi 17.


Amesema wakati anachukua madaraka kufuatia kifo cha mtangulizi wake, dunia ilikuwa ikikabiliwa na mlipuko mkubwa wa Covid 19, nchi nyingi ziliathirika kiuchumi, hata Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika, ambapo uchumi wake uliporomoka kutoka asilimia  6.9 hadi asilimia  4.7.

“Tunavyoongea hapa, katika kipindi changu cha mwaka mmoja uchumi umepanda na kufikia asilimia 5.2, matarajio yangu ni kufikia asilimia 6 mwaka 2025,” amesema.

Habari leo
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger