Ticker

6/recent/ticker-posts

Sauti Sol Kumshtaki Raila Odinga kwa madai ya Kutumia Wiimbo Wao Kwenye Kampeni za Siasa

 


Kundi la muziki nchini Kenya Sauti Sol limetishia kushtaki kampeni za urais za Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga kwa madai ya ukiukaji wa hakimiliki.


Akaunti za mitandao ya kijamii za Odinga zinasemekana kutumia wimbo wa Sauti Sol wa Extravaganza wakati wa kumtambulisha Martha Karua kama mgombea mwenza wa Muungano wa Azimio la Umoja.


Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter, Sauti Sol walilalamika kuhusu matumizi ya muziki wao katika kampeni zinazoendelea za kisiasa.


Walisema “hawakuwa na uhusiano wala kuhusishwa na kampeni ya Azimio la Umoja au vuguvugu lolote la kisiasa na/au chama”.


“Tumesikitishwa na kampeni ya Azimio la Umoja ya kupuuza waziwazi haki yetu ya kudhibiti matumizi ya hakimiliki yetu.”

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments