5/18/2022

Sauti Sol Wakosolewa Vibaya Baada ya Nia yao Kumshitaki Rails Odinga Kutumia Wimbo Wao, Tanzania Yatolewa Mfano Mzuri

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


“Tanzania wasanii kama Diamond Platnumz, AliKiba, Harmonize, Zuchu, Nandy na wengine wanashindana ni yupi ameachia wimbo mzuri kwa Mgombea wa Urais. Hapa Kenya Sauti Sol kusafiri kidogo tu kwenda Ulaya, wanaanza kujiona kama wao ndio wanampa uhai Mwanasiasa ambaye alitumia wimbo wao.” Wahinya Charlie.


Wiki hii bendi maarufu nchini Kenya Sauti Sol imetishia kukishtaki Chama cha Azimio la Umoja kwa kutumia wimbo wao “Extravaganza” bila ridhaa yao kwenye kampeni zao ambapo siku hiyo walikuwa wakimtambulisa Mgombea mwenza wa Raila Odinga, Bi. Martha Karua.


Sauti Sol wamekuwa wakipokea ukosoaji mkubwa kwenye mitandao ya Kijamii na taarifa mpya ni kuwa wamepoteza Jumla ya Subscribers 2,000 kwenye chaneli yao ya YouTube tangu wachapishe tamko hilo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger