5/20/2022

Sean Paul Afunguka Alivyogombezwa na Beyonce na Kukatiwa Mawasiliano Kimoja

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

Katika mahojiano mapya Sean Paul(49) amesema aliwahi kugombezwa na Beyonce(40) baada ya uvumi kuanza kuenea kuwa wao ni wapenzi kufuatia colabo yao ya wimbo wa "Baby Boy" uliotoka 2003 kufanya vizuri sana sokoni

Wimbo huo wa Beyonce kuwa superhit ulifanya wawili hao kuutumbuiza pamoja katika shows mbalimbali kubwa lakini uvumi ulipoanza kuwa wao ni wapenzi Beyonce hakupendezwa ambapo Sean Paul alimjibu Beyonce kuwa yeye hahusiki kueneza uongo huo kuwa ni wapenzi ila Beyonce alitaka uvumi huo lazima utoweke haraka iwezekanavyo

Beyonce aliona uvumi huo utamharibia career yake ya muziki na baada ya hapo Sean Paul na Beyonce hawakuweza kuutumbuiza tena pamoja wimbo huo wala kuwa karibu tena Kama ilivyokuwa kabla

Sean Paul alipoulizwa kuwa labda Jay Z na management ya Beyonce walihusika kuwaweka mbalimbali, akajibu hana uhakika kuhusu hilo

Hata hivyo, katika mahojiano hayo Sean Paul amesema Beyonce ni mwanamke mzuri sana na anatamani wangekuwa wapenzi kweli kama ilivyoanza kuvumishwa kipindi hicho

Pia Sean Paul amesema, alipofuatwa na Beyonce wafanye pamoja wimbo wa Baby Boy alifurahi sana
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger