Siku ya mama:Mateso Aliyopitia Mama wa Trevor Katika UchekeshajiMchekeshaji maarufu kutoka Afrika ya kusini Trevor Noah alipokuwa akiandika kitabu chake kiitwacho ‘Born a Crime’, alitaka kuudhihirishia ulimwengu kuwa yeye ni shujaa, lakini wakati wa mchakato wa kukiandika kitabu hicho, aligundua kwamba heshima na ushujaa aliotaka kujivika yeye ulipaswa kwenda kwa kwa mama yake mzazi Patricia.


“Nilifikiri kwamba nilikuwa shujaa wa hadithi yangu, lakini katika kuiandika nilikuja kutambua baada ya muda kuwa mama yangu ndiye shujaa,” Trevor alisema kauli hiyo mwaka 2016.


Patricia Noah ambaye ndio mama mzazi wa Trevor alikulia Afrika Kusini wakati huo nchi hiyo ilikuwa chini ya sheria ya ubaguzi wa rangi, mfumo wa ubaguzi uliodumu kwa miaka isisyopungua 50.


Chini ya ubaguzi wa rangi, Patricia alijikuta hatarini kiasi cha kunusurika kufungwa gerezani kutokana na kumzaa Trevor ambaye baba yake alikuwa mzungu.


Hofu ya kufungwa gerezani ilimlazimu kumlea Trevor kwa usiri mkubwa ili kuficha asibainike kuwa na mtoto wa kizunngu.


“Bibi yangu alinifungia ndani ya nyumba nilipokuwa nikiishi na familia huko Soweto,” alisema Trevor.


Alipokuwa akiendelea kukua inaelezwa mara nyingi Patricia ilimbidi kujifanya hawajuani na mwanae akiwa hadharani, ili kuepuka isitokee akakamatwa.


“Mama yangu alikuwa mcheshi wa kwanza wa kweli niliyewahi kumuona, Yeye ni kama mcheshi unapozungumza naye, anavuta nyuso, anabadilisha sauti yake, kimwili, angeweza kufanya mambo ya kuchekesha. Anastarehesha sana ukiwa naye, zilikuwa talanta za asili ambazo alikuwa nazo na akanipitishia mimi. Nadhani ndio sababu napenda vichekesho sana” alisema Trevor.


Trevor Noah ni mcheshi maarufu kutoka Afrika ya kusini na mtangazaji wa kipindi cha Vichekesho cha The Daily Show, historia ya maisha yake inamzungumzia kijana aliyepitia mengi hata hivyo anamuhusisha mama yake katika yote aliyoyapitia pamoja na mafanikio yake, akiisifu nguvu na ujasiri wake

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad