Simba Anaendelea Kumsafishia Yanga Kiti cha Ubingwa, Namungo Wamshika Break


Imeandikwa na @swalehmawele

FT: Namungo FC 2-2 Simba SC

🔊 Simba anaendelea kumsafishia Yanga njia ya kuelekea kwenye kiti cha ubingwa, wamekusanya alama tatu katika mechi tatu za mwisho, sare tatu mfululizo, hiyo ni hatari kwao na ni faida kwa mpinzani wake wa karibu ( Yanga ).

🔊 Simba wamedondosha alama katika mechi nyepesi mbele ya Namungo, hawakucheza dhidi ya mpinzani ambae aliwazidi kwenye vitu vingi ndani ya kiwanja, utofauti ulikuja katika usahihi wa Namungo kwenye matendo ya mwisho.

🔊 Namungo walichagua kucheza zaidi katika low block defensive system na wakizitumia zaidi counter attacks ( mashambulizi ya kushitukiza ), ilikuwa ni ngumu kwao katika set play kwa sababu mara nyingi walizidiwa idadi ya wachezaji, 2 vs 3 au 1 vs 3.

🔊 Simba ni kama ilikosa maarifa na uthubutu katika kuitumia zonal 14, walizichagua wide areas na kutumia mipira ya krosi, tatizo likaja kwao baada ya Namungo kufanikiwa kucheza mipira mingi ya juu, walizuia vyema sana.

✅ Sina takwimu sahihi lakini inawezekana huu ukawa ni msimu ambao Simba amefungwa magoli mengi ya krosi.
✅ Reliant Lusajo, wow, mtulivu na uthubutu, anacheza nyuma ya mshambuliaji kwa usahihi mkubwa sana.
✅ Simba hawana benchi, wanaoingia hawaleti kitu cha tofauti ndani ya kiwanja.
✅ Ni busara kwa Simba kama watawekeza nguvu kwenye ASFC, huku kwenye ligi nafasi ni ndogo mno.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad