Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Kwa Sasa Inatakiwa Kuanza Upya Kulinda Heshima yao

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>
Na @EmanuelMwayomboJr

Simba Sports Club kwa sasa inatakiwa kuwekeza nguvu kubwa kuelekea msimu ujao ili iwe na kikosi imara cha kushindana katika Ligi pia katika michuano ya Kimataifa.

Simba Sports Club lazima watafute nyota wengine wapya wa kiwango cha juu zaidi ambao watawavusha kutoka hatua ya Robo Fainali kule katika Michuano ya CAF hadi Nusu fainali ya Michuano ile kwa sababu kwa aina ya wachezaji walionao hivi sasa siwaoni Simba wakipenya zaidi ya Robo hata kama wataendelea kuwa nao.

Simba wanapofanya usajili wanatakiwa kuangalia mbali zaidi kwa kusajili mchezaji ambaye atakuja katika Klabu yao na kuwaongezea nguvu katika michuano ya Kimataifa ili waendelee kulinda heshima yao katika michuano ile.

Unaweza ukafanya usajili mzuri lakini ukawa usajili wa kushindana hapa ndani tu lakini linapokuja suala la International Competition wewe unageuka njia ya watu kuvuka na kwenda hatua inayofuata.

Ili ndoto ya Simba itimie lazima waende sokoni kununua wachezaji wa kiwango cha juu zaidi ambao watawavusha kutoka Robo Fainali hadi kusogea mbele zaidi kwa sasa Simba hawatakiwi kumwangalia usoni mtu kama ameshindwa kuleta mafanikio mliyo yategemea katika kikosi chenu achana naye leta wengine ambao wataisogeza timu mbele zaidi.

Kumbuka kila kitu kinapojengwa wengi huhusika katika ujenzi lakini watakao faidi ni wengine Simba kwa sasa hawana budi kubomoa kikosi Chao kwa mafanikio zaidi Kimataifa.

Ili Ndoto ya Simba itimie Kimataifa kutinga Nusu Fainali ama Fainali lazima hiki kikosi cha sasa wabaki wachezaji wachache tu, zije sura nyingi mpya za kuleta kitu kipya ndani ya Klabu hii hawa wa sasa hawatawafikisha mbali kama ambavyo wao wanataka.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments