Ticker

6/recent/ticker-posts

Sintofahamu Maharusi Wakijiteketeza Moto Bila Kuchomeka Wakati wa Harusi yaoWanandoa hao, Ambyr Bam na Gabe Jessop, ambao wanasemekana kuwa wasanii wenye vipaji vya kustaajabisha, waliwasisimua wageni wao na mchezo wa kutisha
Wanandoa hao walijiteketeza moto wakati walikuwa wakiondoka kwenye harusi yao
Katika video, maharusi hao walivalia mavazi na suti zisizoshika moto, waliteketezwa moto kabla ya baadaye kuzimwa na kifaa cha kuzimia moto
Maharusi waliobadilishana viapo vya ndoa hivi majuzi, waliwaacha wageni wao wakiwa wamepigwa na butwaa baada ya kufanya vimbwanga visivyokuwa vya kawaida wakati wa sherehe ya harusi yao.

Maharusi Wazua Hofu Baada ya Kujiteketeza Moto Wakati wa Harusi yao
Maharusi Wazua Hofu Baada ya Kujiteketeza Moto Wakati wa Harusi yao Picha: Russ Powell.
Wanandoa hao, Ambyr Bam na Gabe Jessop, ambao wanasemekana kuwa wasanii wenye vipaji vya kustaajabisha, waliwasisimua wageni wao kwenye sherehe iliyoongozwa na filamu ya Hunger Games.

Sawia na namna waigizaji katika filamu maarufu ya Hollywood, Hunger Games na Catching Fire, hujiteketeza moto, wanandoa hao pia walijiwasha moto wakati walikuwa wakiagwa kwenye harusi yao.

Baada ya mapokezi yao, maharusi hao waliovalia mavazi na suti zisizoshika moto, waliteketezwa moto kabla ya kuingia uwanjani wakiwa na miale ya moto migongoni mwao, ambayo baadaye ulizimwa na kifaa cha kuzimia moto.


 
Kwa Nini Martha Karua Ndiye Changuo Bora Zaidi kuwa Mgombea Mwenza wa Raila
Video ya tukio hilo la kuvutia ilishirikiwa kwenye mtandao wa TikTok na mmoja wa wageni wao, Russ Powell, na akanukuu: "Ambyr na Gabe walikutana kwenye seti, kuondoka kwa harusi yao kunafanya fataki kuonekana kuwa ya kuchosha."

Hata hivyo alionya watu dhidi ya kujaribu kufanya hivyo kwenye harusi zao bila kuchukua hatua zinazofaa za usalama, akibainisha kuwa wanandoa hao ni wataalamu waliohitimu.

Akijibu maoni ya baadhi ya wanamtandao ambao walishangazwa kuwa wanandoa hao hawakuungua licha ya joto kali la moto, Russ alisema: "Wote walikuwa na jeli ya kuzuia kuungua kwenye nywele na usoni, kisha Ambyr alikuwa na wigi juu. .”

Tazama video hiyo hapa

Bwana Harusi avunjika mgongo baada ya marafiki kumrusha
Katika taarifa tofauti, bwana harusi aligeuka kuwa mgonjwa katika hafla yake ya harusi baada ya kuangukia kichwa chake.

Kisa hicho kilitokea katika harusi moja kaunti ya Bihor, Kaskazini Magharibi mwa Romania Septemba 2021.

Kwa mujibu wa The Sun, bwana harusi huyo aliporushwa hewani mara ya kwanza, alidakwa lakini katika jaribio la pili aliangukia kichwa na kumsababishia jeraha mbaya.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments